sahini

sahini

Thursday, August 28, 2014

ARSENAL YAPONEA CHUPU CHUPU UEFA.

Video: Arsenal yapenya kwa mbinde, Mathew Debuchy alambwa kadi nyekundu

posted 6 hours ago by admin
Mzimu wa kadi nyekundi umeendelea kuisumbua Arsenal katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya ambayo usiku wa kuamkia hii leo ilimaliza hatua ya michezo ya mtoano.
Arsenal walijikuta wakimaliza pungufu walipokuwa katika uwanja wao wa nyumbani wakicheza mchezo wa mkondo wa pili wa hatua ya mtoano dhidi ya Besiktas kutoka nchini Uturuki baada ya beki wao wa pembeni kutoka nchini Ufaransa Mathew Debuchy kuonyeshwa kadi mbili za njano ambazo zilizaa kadi nyekundu.
Hata hivyo kabla ya tukio hilo halijatokea katika dakika ya 75 Arsenal walikuwa mbele kwa bao moja ambalo liliwapa ushindi wa jumla na kufanikiwa kusonga mbele kwenye hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Bao hilo pekee na la ushindi lilifungwa na mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Chile Alexis Alajandro Sanchez katika dakika ya 45 kipindi cha kwanza.
Mara baada ya mtanange huo kumalizika huko kaskazini mwa jijini London meneja wa Arsenal, Arsene Wenger aliteta na waandishi wa habari na kuelezea ugumu wa mpambano huo ulivyokuwa hasa baada ya muamuzi kutoka nchini Ureno Pedro Proença Oliveira Alves Garcia kumuadhibu kwa kadi nyekundu Mathew Debuchy kufuatia madhambi aliyomfanyia Mustafa Pektemek.
Wenger amesema kwa hakika muamuzi Proenca hakumtendea haki Debuchy kwa kumuadhibu kwa kadi nyekundi kutokana na uhalisia ulioonekana kwa kuucheza mpira na si kumfanyia madhambi Mustafa Pektemek.
Ushindi huo wa bao moja kwa sifuri ambao unaoivusha Arsenal hadi katika hatua ya makundi, unampa sifa kubwa meneja Arsene Wenger kutokana na mafanikio ya kuiwezesha klabu hiyo ya jijini London kucheza michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya kwa mara ya 17 mfululizo tangu alipoajiriwa mwaka 1996

No comments:

Post a Comment