sahini

sahini

Thursday, September 4, 2014

USAJILI WA MANCHESTER UNITED: VAN GAAL MWANAJESHI ANAYEKUMBATIA BUNDUKI YENYE MITUTU MIWILI……


1409747838407_wps_6_MANCHESTER_ENGLAND_SEPTEM
Na Nicasius Coutinho Suso
Moja ya wanadamu wanapata kujifanyia utalii kila mwaka pasi na wao kufahamu ni mwanamama Lorelei Taron. Wengi hawamjui huyu, lakini huyu ndie mwanamama anayezipendeza vyema na kuzing’arisha ipasavyo mboni za Radamel Falcao, namaanisha ndio mkewe. Kutokana na Maisha ya mumewe ana uhakika wa kuwa na pasi ya kusafiria kwenda nchi tofauti kila mwaka.
Ndio hata juzi kasafiri tena, katika siku tulivu kabisa yeye alikuwa anapata kahawa nje kidogo ya nyumba  akisubiri dili la mume wake kukamilika kutua Manchester United. Pengine huu ndio usajiri ambao haukutarajiwa na wengi ila umetokea, wakati wengi wakimuwaza Vidal, Van Gaal alifanya biashara ya kikubwa na Arsene Wenger, huku akampeleka Welbeck yeye akamuingiza Falcao. Alichofanya Van Gaal ni sawa na kuleta keki msibani.
Wakati mashabiki wengi wa United wakiwa wanalia na Beki ama,Kiungo mkabaji wa asili, yeye hajawaza sana, amewaletea kile kitu ambacho ni kitamu mdomoni, kitu ambacho ukiwaza Mara mbili unakikumbatia Mara mbili Kisha unasema Ahsante Mungu kwa siku hii. Hii ni saikolojia nzuri sana ya Ed Woodward na Van Gaal.
1409737559630_wps_4_ST_ALBANS_ENGLAND_SEPTEMBDanny Welbeck alitua Arsenal
Naamini walijua mapema kabisa Arturo Vidal hasingeweza/hatoweza kufika, sasa kilichotakiwa ni kufanya Marquee signing(usajiri mkubwa) Kisha kuondoa wale wanaonekana ni wasiotakiwa pale. Lakini pamoja na hayo hili hupaswa kufanywa kwa mahesabu makali sana, mahesabu ya kulenga shabaha pin iliyoning’inia katika uzi.
Unajua kwanini mahesabu ya Van Gaal yamefanya kazi kwa mashabiki.? Hawawazi namna ya kumzuia Aguero tena kama Liverpool walivyoshindwa Bali wanawaza namna ipi watakabwa wao. Wanawaza baada ya wiki hii ya mechi za kimataifa wao ndio watakuwa paka wa kuvikwa kengele. Usiwazuie kuwaza hivyo wapo sahihi sana.
Kwa sasa Carlington katika mazoezi wamepishana watu wawili Mlangoni, watu tofauti lakini wenye Nia moja. Wote wana kazi ya kufunga magoli katika timu zao. Carlington kwa sasa lile eneo alilokuwa anafanyia mazoezi Welbeck atakuwepo Radamel Falcao.
Hapa ndipo mashabiki wanapopata faraja, hapa ndipo Carlington inapopendeza, hapa ndipo Mata anapofarijika, na hapa ndipo Di Maria anapohitaji. Zile Rabona zake zitaelekea katika miguu ya moja ya washambuliaji hatari wa Dunia hii.
Hapa ndipo hata Kompany anapoanza kuiwaza Derby pia. Unawaza kupambana na Falcao, Rooney, Van persie, Di Maria na Mata kabla hujawaza Aguero atafanya nini. Katika miaka ya karne ya 18 huko Pressia ambayo kwa sasa ni Ujerumani. Alipata kuzaliwa mtu anaitwa Carl Von Clausewitz. Huyu alikuja kuwa mwanafilosofia mzuri wa masuala ya jeshi.
Huyu ndio chanzo cha filisofia za “ON WAR” yaani KATIKA VITA. Katika moja ya vitu anavyoaminika kuwa ndiye mwanzilishi ni ule usemi maarufu wa “THE BEST DEFENSE IS GOOD OFENSE”. Maana yake njia bora ya kujilinda ni ushambuliaji mzuri.
gaalKocha wa Manchester United, Louis van Gaal
Na hapa ndipo namwona Louis Van Gaal na Machester United, hapa ndipo nayaona mahesabu yake ya kulenga shabaha pin yalipo. Baada ya kukosa mahitaji ya ulinzi akaamua kuwekeza katika ushambuliaji, akaamua kufanya uamuzi wa kuwapishanisha Welbeck na Falcao mlangoni.
Na hapa ndipo unapowatizama Manchester united, wakiwa fiti wana safu ya ushambuliaji imara kuliko Bayern Munich. Lakini alichokifanya Van Gaal ni kama mwanajeshi anayemiliki bunduki yenye mitutu miwili. Anatakiwa kuwa makini katika utumiaji wake. Anatakiwa mahesabu mengine bora na fanisi zaidi ya yale ya kulenga shabaha pini. 
Baada ya mashabiki kuamini kuwa sasa ni tishio, Van Gaal anatakiwa kumuishi Von Clausewitz, anatakiwa kuifanya safu ya ushambuliaji iwe ngao yake ya kujilinda, anatakiwa awafanye Kompany, Skrtel, Koscielny, Cahill wamuogope kabla hajawaogopa akina Diego Costa.
Na hapa ndipo kamali ilipo, na hapa ndipo Van Gaal anapojikuta kakumbatia Bunduki yenye mitutu miwili. Inahitaji umakini katika upigaji wake, mtutu mmoja upo uelekeo wa adui mwingine unaelekea kwake mwenyewe. Akikosea namna ya kuruhusu risasi itampata yeye na kumwacha adui salama. Akipatia ameshinda vita.
Naisubiri Mei sasa, nasubiri kuona ulengaji wake, akiipatia tunaweza kumuona LORELEI TARON akiacha utalii wake akatulia pale Manchester, akikosea itamjeruhi mwenyewe na Sioni kama atabaki salama pale, tuataandaa Visa yake na ya LORELEI kwa Mara nyingine, na hapa ndio Urafiki wa Perez na Mendez utaongezeka. Ndio maana watakuwa wanapata Jack Daniels huku wanajadili namna ya kumpata Falcao tena. Ahsanteni

1 comment:

  1. ATZ Sport has been my go-to for watching live sports. Highly recommend their website for sports enthusiasts.

    ReplyDelete