sahini

sahini

Thursday, September 4, 2014

USAJILI WA MANCHESTER UNITED: VAN GAAL MWANAJESHI ANAYEKUMBATIA BUNDUKI YENYE MITUTU MIWILI……


1409747838407_wps_6_MANCHESTER_ENGLAND_SEPTEM
Na Nicasius Coutinho Suso
Moja ya wanadamu wanapata kujifanyia utalii kila mwaka pasi na wao kufahamu ni mwanamama Lorelei Taron. Wengi hawamjui huyu, lakini huyu ndie mwanamama anayezipendeza vyema na kuzing’arisha ipasavyo mboni za Radamel Falcao, namaanisha ndio mkewe. Kutokana na Maisha ya mumewe ana uhakika wa kuwa na pasi ya kusafiria kwenda nchi tofauti kila mwaka.
Ndio hata juzi kasafiri tena, katika siku tulivu kabisa yeye alikuwa anapata kahawa nje kidogo ya nyumba  akisubiri dili la mume wake kukamilika kutua Manchester United. Pengine huu ndio usajiri ambao haukutarajiwa na wengi ila umetokea, wakati wengi wakimuwaza Vidal, Van Gaal alifanya biashara ya kikubwa na Arsene Wenger, huku akampeleka Welbeck yeye akamuingiza Falcao. Alichofanya Van Gaal ni sawa na kuleta keki msibani.
Wakati mashabiki wengi wa United wakiwa wanalia na Beki ama,Kiungo mkabaji wa asili, yeye hajawaza sana, amewaletea kile kitu ambacho ni kitamu mdomoni, kitu ambacho ukiwaza Mara mbili unakikumbatia Mara mbili Kisha unasema Ahsante Mungu kwa siku hii. Hii ni saikolojia nzuri sana ya Ed Woodward na Van Gaal.
1409737559630_wps_4_ST_ALBANS_ENGLAND_SEPTEMBDanny Welbeck alitua Arsenal
Naamini walijua mapema kabisa Arturo Vidal hasingeweza/hatoweza kufika, sasa kilichotakiwa ni kufanya Marquee signing(usajiri mkubwa) Kisha kuondoa wale wanaonekana ni wasiotakiwa pale. Lakini pamoja na hayo hili hupaswa kufanywa kwa mahesabu makali sana, mahesabu ya kulenga shabaha pin iliyoning’inia katika uzi.
Unajua kwanini mahesabu ya Van Gaal yamefanya kazi kwa mashabiki.? Hawawazi namna ya kumzuia Aguero tena kama Liverpool walivyoshindwa Bali wanawaza namna ipi watakabwa wao. Wanawaza baada ya wiki hii ya mechi za kimataifa wao ndio watakuwa paka wa kuvikwa kengele. Usiwazuie kuwaza hivyo wapo sahihi sana.
Kwa sasa Carlington katika mazoezi wamepishana watu wawili Mlangoni, watu tofauti lakini wenye Nia moja. Wote wana kazi ya kufunga magoli katika timu zao. Carlington kwa sasa lile eneo alilokuwa anafanyia mazoezi Welbeck atakuwepo Radamel Falcao.
Hapa ndipo mashabiki wanapopata faraja, hapa ndipo Carlington inapopendeza, hapa ndipo Mata anapofarijika, na hapa ndipo Di Maria anapohitaji. Zile Rabona zake zitaelekea katika miguu ya moja ya washambuliaji hatari wa Dunia hii.
Hapa ndipo hata Kompany anapoanza kuiwaza Derby pia. Unawaza kupambana na Falcao, Rooney, Van persie, Di Maria na Mata kabla hujawaza Aguero atafanya nini. Katika miaka ya karne ya 18 huko Pressia ambayo kwa sasa ni Ujerumani. Alipata kuzaliwa mtu anaitwa Carl Von Clausewitz. Huyu alikuja kuwa mwanafilosofia mzuri wa masuala ya jeshi.
Huyu ndio chanzo cha filisofia za “ON WAR” yaani KATIKA VITA. Katika moja ya vitu anavyoaminika kuwa ndiye mwanzilishi ni ule usemi maarufu wa “THE BEST DEFENSE IS GOOD OFENSE”. Maana yake njia bora ya kujilinda ni ushambuliaji mzuri.
gaalKocha wa Manchester United, Louis van Gaal
Na hapa ndipo namwona Louis Van Gaal na Machester United, hapa ndipo nayaona mahesabu yake ya kulenga shabaha pin yalipo. Baada ya kukosa mahitaji ya ulinzi akaamua kuwekeza katika ushambuliaji, akaamua kufanya uamuzi wa kuwapishanisha Welbeck na Falcao mlangoni.
Na hapa ndipo unapowatizama Manchester united, wakiwa fiti wana safu ya ushambuliaji imara kuliko Bayern Munich. Lakini alichokifanya Van Gaal ni kama mwanajeshi anayemiliki bunduki yenye mitutu miwili. Anatakiwa kuwa makini katika utumiaji wake. Anatakiwa mahesabu mengine bora na fanisi zaidi ya yale ya kulenga shabaha pini. 
Baada ya mashabiki kuamini kuwa sasa ni tishio, Van Gaal anatakiwa kumuishi Von Clausewitz, anatakiwa kuifanya safu ya ushambuliaji iwe ngao yake ya kujilinda, anatakiwa awafanye Kompany, Skrtel, Koscielny, Cahill wamuogope kabla hajawaogopa akina Diego Costa.
Na hapa ndipo kamali ilipo, na hapa ndipo Van Gaal anapojikuta kakumbatia Bunduki yenye mitutu miwili. Inahitaji umakini katika upigaji wake, mtutu mmoja upo uelekeo wa adui mwingine unaelekea kwake mwenyewe. Akikosea namna ya kuruhusu risasi itampata yeye na kumwacha adui salama. Akipatia ameshinda vita.
Naisubiri Mei sasa, nasubiri kuona ulengaji wake, akiipatia tunaweza kumuona LORELEI TARON akiacha utalii wake akatulia pale Manchester, akikosea itamjeruhi mwenyewe na Sioni kama atabaki salama pale, tuataandaa Visa yake na ya LORELEI kwa Mara nyingine, na hapa ndio Urafiki wa Perez na Mendez utaongezeka. Ndio maana watakuwa wanapata Jack Daniels huku wanajadili namna ya kumpata Falcao tena. Ahsanteni

MANCHESTER UNITED HAWAKUPOTEA NJIA, DI MARIA ATENGENEZA MATATU NA KUJIPIGIA MOJA ARGENTINA IKIICHAPA UJERUMNAI 4-2


1409775941982_wps_28_Argentina_s_Angel_Di_Mari
ANGEL di Maria alionesha uwezo wake wa kutandaza kabumbu baada ya kutengeneza magoli matatu na kufunga moja, Argentina akiwatandika 4-2 mabingwa wa dunia, Ujerumani.
Nyota huyo aliyevunja rekodi ya usajili ya Manchester United alitoa pasi za mwisho za magoli ya Sergio Aguero, Erik Lamela na Federico Fernandez kabla ya kufunga la kwake ikiwa ni kulipa kisasi cha kufungwa bao 1-0 katika fainali ya kombe la dunia ambapo bao la dakika za nyongeza la Mario Gotze lilizima ndoto za Argentina kutwaa kombe la dunia majira ya kiangazi mwaka huu nchini Brazil. 
Nyota wa Mchezo: Angel di Maria alionesha kiwango cha hali ya juu.
Magoli matano kati ya sita yaliyofungwa jana mjini Dusseldorf yalifungwa na wachezaji wanaocheza ligi kuu England ambapo moja la Ujerumani lilifungwa na Andre Schurrle anayekipiga Chelsea na lingine likatiwa kimiani na Gotze.

WAYNE ROONEY AITENDEA HAKI BEJI YA UNAHODHA, AIPIGIA MOJA ENGLAND IKIICHARAZA 1-0 NORWAY


1409776336221_wps_34_SPT_GCK_030914_Football_E
Kamwe hana wasiwasi: Nahodha wa England ,Wayne Rooney akifunga goli kwa mkwaju wa penalti na kuipa timu yake bao la kuongoza katika uwanja wa nyumbani wa Wembley dhidi ya Norway.
All smiles: Rooney is congratulated after scoring the winner for England in their first match since returning from the World Cup 
Kikosi cha England: Hart 6, Stones 6.5 (Chambers 81), Jones 6.5, Cahill 6.5 (Jagielka 84), Baines 6, Oxlade-Chamberlain 6 (Delph 69, 6), Henderson 6, Wilshere 6.5 (Milner 69, 6), Sterling 7.5, Rooney 6.5 (Welbeck 70, 6), Sturridge 6.5 (Lambert 89).
Wachezaji wa akiba: Forster, Rose, Townsend. 
Goals: Rooney 68.
Kikosi cha Norway: Nyland 6, Elabdellaoui 5.5, Nordtveit 6, Forren 6, Linnes 5 (Flo 36, 6), Skjelbred 6.5 (Elyounoussi 69, 6), Johansen 6.5, Jenssen 6 (Pedersen 87), Daehli 6 (Konradsen 57, 6), King 6 (Nielsen 76), Elyounoussi 6 (Kamara 78).
Wachezaji wa akiba: Jarstein, Semb Berge, Hagen, Samuelsen, Tettey, Mohamed Elyounoussi, Hansen.
Mwamuzi: Jorge Sousa (Porto).
Watazamaji: 40,181. 

KIPUTE CHA NGAO YA JAMII BAINA YA YANGA NA AZAM FC CHASOGEZWA MBELE


_DSC0064
MECHI ya Ngao ya Jamii kuashiria kufunguliwa kwa pazia la ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2013/2014 baina ya mabingwa Azam fc na makamu bingwa, Dar Young Africans sasa utapigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam septemba 14 badala ya septemba 13 mwaka huu kama ilivyopanga.
Shirikisho la soka Tanzania limeamua kuusogeza kwa siku moja mchezo huo uliotakiwa kupigwa jumamosi na sasa kupigwa jumapili kwa lengo la kuwapa fursa mashabiki wengi kuuona.
TFF imesema jumapili ni siku tulivu kuliko jumamosi na mchezo wa mwaka huu utaambatana na shughuli za kijamii ikiwemo uchangiaji wa damu.
Pia sehemu ya mapato ya mchezo huo yatapelekwa katika shughuli ya kijamii iliyochaguliwa.
Mechi hiyo itapigwa ikiwa ni wiki moja kabla ya kuanza kwa ligi kuu septemba 20 mwaka huu ambapo Yanga wataanzia ugenini dhidi ya Mtibwa Sugar katika dimba la Jamhuri mkoani Morogoro.
Mnyama Simba atakuwa uwanja wa Taifa siku moja baada ya kufunguliwa kwa ligi kuu (septemba 21 mwaka huuu) dhidi ya Wagosi wa Kaya, Coastal Union.
Azam fc watakuwa nyumbani Azam Conmplex kuchuana na Polisi Morogoro.

GOR MAHIA WATUA KUJARIBU MAKALI YA SIMBA SC


Gor-Mahia-24102012
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
WEKUNDU wa Msimbazi wanatarajia kucheza mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya mabingwa wa ligi kuu nchini Kenya, Gor Mahia siku ya jumamosi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Geofrey Nyange ‘Kaburu’, makamu wa Rais wa Simba sc, amewaambia waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuwa kikosi cha Gor Mahia kitawasili kesho uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam kikitokea Nairobi kwa kutumia ndege ya shirika la Kenya.
Kaburu aliongeza kuwa nacho kikosi cha Simba kitawasili siku hiyo hiyo kikitokea Zanzibar kilipoweka kambi ya kujiwinda na ligi kuu.
Licha ya kukipiga na Simba, Gor Mahia imeomba kucheza mechi mbili, hivyo siku ya jumapili watakuwa na mechi nyingine ya kirariki wakati kikosi cha Patrick Phiri kitarejea Zanzibar kuendelea kumalizia program zake za maandalizi kabla ya ligi kuanza septemba 20 mwaka huu.
Awali Simba walipanga kuchuana na Mtibwa Sugar, lakini kocha Phiri akapendekeza kutafutiwa mechi ngumu ya kimataifa ili kuangalia namna kikosi chake kilivyoimarika.
Mechi ya jumamosi itakuwa fursa nzuri kwa mashabiki wa Simba kuwaona wachezaji wao akiwemo mshambuliaji hatari aliyerejea Msimbazi, Mganda Emmanuel Anord Okwi ambaye atavalia jezi yake namba 25 aliyokuwa anaitumia kabla ya kutimkia Etoile Du Sahel ya Tunisia.
Kaburu alisema viingilio katika mechi hiyo ni shilingi elfu 5 (5,000) kwa viti vya kijana, viti vya rangi ya chungwa ni shilingi 10,000, VIP C na B itakuwa shilingi 2,000 wakati VIP A itakuwa shilingi elfu 30,000.
Tiketi kwa ajili ya mchezo huo zitaanza kuuzwa siku ya mechi kuanzia majira ya saa 4:00 asubuhi.
Simba wataanza kampeni za kusaka ubingwa wa ligi kuu bara septemba 21 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam dhidi ya Coastal Union.

MBEYA CITY FC KUJIPIMA MAKALI NA BIG BULLETS


Mbeya-City
 Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam,
 Ili kujiimarisha zaidi kuelekea msimu mpya wa ligi kuu Tanzania Bara, klabu ya Mbeya City inataraji kucheza michezo miwili ya kimataifa ya kirafiki kabla ya kuanza kwa msimu mpya Septemba 20 ambapo timu hiyo iliyomaliza katika nafasi ya tatu msimu uliopita itafungua dimba dhidi ya ‘ Maafande’  wa JKT Ruvu katika uwanja wa Sokoine, Mbeya.
 Kocha mkuu wa timu hiyo, Juma Mwambusi ameuagiza uongozi wa timu hiyo kumtafutia michezo miwili dhidi ya klabu za Malawi.
 Big Bullets ni klabu kongwe nchini Malawi na Kusini mwa bara la Afrika itacheza na City katika mchezo wa kwanza wa kimataifa.
  ” Nimeuambia uongozi wangu nahitaji mechi mbili ngumu za kimataifa na timu kutoka nchini Malawi. Tunataraji kucheza na Big Bullets ya Malawi ili kujiimarisha zaidi kabla ya kuanza kwa msimu mpya” alisema, Mwambusi.
 City imefanikiwa kuwabakisha kikosini wachezaji wake nyota kama, Paul Nongwa, Saad Kipanga, Hassan Mwasapili, na golikipa, David Baruani licha ya wachezaji hao kuwaniwa na timu kubwa katika dirisha la usajili.
 Mwagane Yeya, Eric Banda wataungana na nyota mpya, Themi Felix kuifanya timu hiyo kuendelea kuwa bora katika msimu wake wa pili katika ligi ya Tanzania Bara.

CRISTIANO RONALDO AFUNGUKA YA MOYONI KUHUSU MANCHESTER UNITED


Kimataifa

1409770800044_wps_24_SPT_GCK_010914_Football_F
Cristiano Ronaldo anatamani kurudi Old Trafford
MWANASOKA bora wa dunia na Ulaya, Cristiano Ronaldo bado ana mapenzi ya dhati na klabu yake ya zamani ya Manchester United.
Ronaldo katika maisha yake hawezi kuisahau United na amesema anaipenda kutoka moyoni mwake.
 “Naipenda Manchester,” alisema. “Kila mtu anajua hilo–na nimesema mara nyingi”.
“Manchester iko moyoni mwangu. Niliwaacha marafiki wengi pale, mashabiki wake ni waajabu na natamani kurudi siku moja”.